Social Icons

BURUDANI SIKU ZOTE

Sample Text

Tuesday, December 18, 2012

MTOTO ACHARANGWA MAPANGA NA BABA YAKE WANACHI NAO WALISANUKISHA


                                                       Marehem  Gift Mustapha 
                                                Mwili waMarehemu ukienda kuzikwa
                                                  Waombolezaji

            Baba wa marehemu ambaye ndiye mtuhumiwa, Mustapha Mchele   
                                      Mama mzazi wa marehemu Gift Mustapha.

Ni mtoto mdogo lakini alikuwa na uwezo mkubwa wa kuchanganua mambo ndiyo maana alipowakuta baba na mama yake wanapigana, haraka sana alihoji sababu ya ugomvi wao, akataka waachiane.
Kumbe baba ni katili, eti swali “kwa nini baba unampiga mama”, likamuudhi, hivyo akamcharanga  mapanga Gift mpaka akapoteza maisha.
Mtoto Gift, ameuawa kikatili mno, picha za tukio tumeshindwa kuzitumia kutokana na maadili, zinaonesha jinsi muuaji alivyomkatakata usoni na kichwa kizima bila huruma.
Gift, aliuawa Desemba 10, 2012, nyumbani kwao, Yombo Buza, Temeke, Dar es Salaam.
Mama wa marehemu, Zulfa Mustapha na majirani zake, wanamlilia Gift, wakimuelezea alikuwa mtoto mzuri, mwenye akili na uwezo mkubwa wa kuchanganua mambo licha ya umri mdogo aliokuwa nao.
SIKU YA TUKIO
Jirani aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, Gift alikuwa anatoka madrasa, alipofika nyumbani aliwakuta wazazi wake wanagombana.
“Ni kawaida ya Gift kufuatawa na ama baba yake au mama yake pindi anapokuwa madrasa lakini siku hiyo hakufuatwa, kwa hiyo alifika nyumbani amechelewa kidogo.
“Inaonekana alisubiri kwa muda kabla ya kuamua kurudi mwenyewe. Akakuta wazazi wake wanagombana, hakujua kama amekikaribia kifo chake.
“Mama yake alikuwa analia, kwa hiyo akamuuliza baba yake ni kwa nini alikuwa anampiga mama yake. Hapohapo, baba mtu akachukua panga na kumcharanga.
“Baada ya kumcharanga mtoto, akamgeukia mkewe, akamkata mkononi na kichwani jeraha moja lakini mama mtu yeye alipata upenyo na kukimbia,” alisema jirani huyo.
MAMA ALIPONA
Ripota wetu, walifanikiwa kumuona Zulfa akiwa na majeraha mawili, moja mkononi na lingine kichwani lakini hali yake ilikuwa inaendelea vizuri.
Hata hivyo, jitihada za maripota wetu kuzungumza na Zulfa ziligonga mwamba kutokana na ndugu zake kuwa wakali.
Wikiendi iliyopita, maripota wetu walifika nyumbani kwake lakini wakaelezwa kwamba ndugu zake wamemhamishia sehemu nyingine.
MTOTO AZIKWA
 Gift, alizikwa Desemba 12, mwaka huu kwenye makaburi ya Yombo Buza, Temeke, Dar es Salaam.
Simanzi ilitanda kwa wakazi wa Yombo, husasan majirani wa familia ya Mustafa Mchele, kwani tukio hilo limekuwa na sura ya aina yake

Majirani wamesema kuwa Mustafa  hakutegemewa na jamii kutenda mauaji hayo kutokana na asili yake ya upole na ukarimu kwa watu.
Wamesema kuwa pia ni mtu anayemjua Mungu vilivyo, kwani husali swala tano.
“Ni msomi, alikuwa akiishi na familia yake vizuri. Tuliposikia mauaji haya tumeshangaa sana, wengi wamehisi kuna mambo ya uchawi hapa,” alisema jirani huyo na kuongeza:
“Wengi wanaamini akili ya Mustafa imechezewa. Katika siku za hivi karibuni kila alipokuwa akienda kazini alikuwa akiumwa, akirejea nyumbani huwa mzima.”
Jirani mwingine ambaye naye aliomba hifadhi ya jina lake, alisema: “Mustafa alikuwa anafanya kazi kwenye kiwanda kimoja kilichopo Barabara ya Nyerere lakini siku za karibuni, alikuwa nyumbani mara nyingi kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
“Kule kiwandani ni kiongozi wa wafanyakazi. Kwa nini aumwe akiwa kazini, akifika nyumbani anapona? Mbona si mtu wa ugomvi, sasa ilikuaje agombane na mkewe kisha amuue mtoto wake kipenzi? Kuna kitu hapa!”
Majirani walisema, Mustafa alikuwa anampenda mno Gift na hata siku ya tukio aliongozana naye mpaka madrasa ambako mtoto huyo alikuwa anasoma
chanzo:
globalpublishers
 

0 comments:

Post a Comment


TUPE SHAVU LAKO FACEBOOK

 

Blogger news

Blogroll

About

This blog is all about providing the correct information from Tanzania and out side the border of Tanzania,the target group is the university and collages student. BURNING ISSUE is all about the hottest news thats hits on that time in Tanzania.