Gari walilopata nalo ajali Salma Salmin ‘Sandra’, Nuru Nassoro ‘Nora’ na Jasmini Nyaku.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wasanii hao walikuwa ndani ya gari aina ya Toyota Fun Cargo lenye namba za usajili T 402 CDU ndipo wakapatwa na msala huo maeneo ya ‘round about’ ya Mlimani City, Dar ambapo gari liliacha njia na kupinduka bila sababu ya msingi.
“Gari halikuwa spidi kiivyo lakini ghafla tukashangaa kuona linagonga ukingo wa barabara na kupinduka ndipo tulipoanza kuwapa msaada na kuwapeleka hospitali,” kilisema chanzo hicho.
Salma Salmin ‘Sandra’.
Nora alipopatikana alifunguka:
“Ilikuwa ghafla tu, tulikuwa mimi, Nyaku, Sandra na mumewe ndani ya gari. Dereva alikuwa Jasmini tukashangaa gari linaacha njia na kupinduka bila sababu yoyote.
“Nimepata majeraha madogomadogo mkononi, Sandra ndiyo aliumia zaidi kichwani, hivyo tulilazimika kumpeleka Hspitali Kwamama Ngoma, Mwenge kisha tukaambiwa tumhamishie Muhimbili alikolazwa hadi sasa hivi.”
Nuru Nassoro ‘Nora’.
CREDIT KWA GLOBAL PUBLISHERS
0 comments:
Post a Comment