Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mh. Godbless Lema ameshinda Rufaa yake ya Ubunge leo Asubuhi na hivyo kuendelea kuongoza jimbo lake la Arusha mjini.
Lema alivuliwa ubunge Aprili 5, 2012 katika hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalira, kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM; Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Habari kamili baadae Kidogo endelea kuperuzi blog yako ya maincampus. Hongereni Chadema na Wanaarusha wote kwa ushindi wa kishindo.
0 comments:
Post a Comment