MKAKATI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kugatua madaraka kwa kutafsiri sera yake ya majimbo, umeanza kazi rasmi katika kanda zake 10, na sasa Kanda ya Ziwa Magharibi imetangaza kikosi kazi kilichosheni wataalamu wa fani mbalimbali.
Kanda hiyo inayohusisha mikoa ya Geita, Kagera na Mwanza, ilizinduliwa wiki iliyopita mkoani Mwanza, mbele ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.
Mkutano wa uzinduzi wa kanda hiyo uliohudhuriwa na wajumbe wa mabaraza ya uongozi, wabunge na madiwani kutoka mikoa hiyo, uliwachagua watu sita kuunda timu ya muda ya uratibu wa kanda kwa miezi mitatu.
Waliochaguliwa kuongoza kanda hiyo ni Peter Mekere (Mwenyekiti), Dk. Rodrick Kabangila (Makamu Mwenyekiti), Renatus Bujiku (Katibu), Cecilia Odemba (Mhazini) na Tungaraza Njugu.
Mekere ni mtaalamu mshauri wa biashara na utawala na mafunzo ya biashara. Ana shahada ya biashara na uongozi na stashahada ya ualimu. Ni mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango ya Shirika la nyumba la Taifa (NHC), Kanda ya Ziwa.
Kabangila ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Afya, Bugando, daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu na Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).
Ana shahada ya uzamili ya magonjwa ya wanadamu, shahada ya udaktari, shahada ya uzamili, epidemilojia na utafiti wa huduma za afya.
CHANZO NI
CHADEMABLOG
0 comments:
Post a Comment