Social Icons

BURUDANI SIKU ZOTE

Sample Text

Tuesday, December 18, 2012

KARIAKOO RISASI ZA RINDIMA MAJAMBAZI YA UA NA KUPORA


Taarifa kamili ni kwamba watu wawili ambao ni Ahmed Mohamed Issa na Sadick Juma wameuwawa kwa risasi december 18 saa nne asubuhi kwenye eneo la tukio la ujambazi Kariakoo Dar es salaam kwenye mitaa ya Livingston na Mahiwa baada ya majambazi kufanya uvamizi ambapo polisi wamefanikiwa kukamata majambazi wanne.
Kamanda Suleiman Kova wa kanda maalum ya Dar es salaam amesema wamiliki wa duka la matairi na betri la Atal Limited walikua na mpango wa kupeleka benki fedha za kitanzania ambazo ni zaidi ya milioni 100 na wakati wanatoka nje wakiwa na fedha majambazi walitokea na pikipiki na kuwataka waingize pesa kwenye gari na kuondoka.
Kamanda Kova amesema wafanyabiashara hao walikaidi amri ya majambazi ambapo waliwapiga risasi wakadondoka hivyo majambazi wakafanikiwa kuchukua pesa lakini wakati wanataka kuondoka alitokea msamaria mwema akiwa na jiwa nae akapigwa risasi na kufariki papo hapo huku mlinzi wa hilo duka aliekua na bunduki akibaki ameduwaa na wala hakujaribu kuitumia bunduki yake.
Kova amesema katika hizo purukushani polisi walimkamata jambazi mmoja akiwa na bastola yenye risasi moja huku majambazi wengine na pikipiki wakikamatwa eneo la tukio wakiwa wamejeruhiwa ambapo kwa sasa wamelazwa katika hospitali ya taifa Muhimbili.

0 comments:

Post a Comment


TUPE SHAVU LAKO FACEBOOK

 

Blogger news

Blogroll

About

This blog is all about providing the correct information from Tanzania and out side the border of Tanzania,the target group is the university and collages student. BURNING ISSUE is all about the hottest news thats hits on that time in Tanzania.