Mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 23 anadaiwa kubakwa na kikundi cha watu ndani ya basi binafsi katika mji wa Delhi.
Polisi wamesema mwanafunzi huyo alikuwa akisafiri na rafiki yake majira ya usiku wakati walipovamiwa na kupigwa na kujeruhiwa vibaya, kuvuliwa nguo na kisha kutupwa nje ya basi hilo.
Wote wawili wamelazwa hospitali kwa matibabu, huku hali ya mwanafunzi huyo ikisemekana kuwa mbaya.
Mji wa Delhi umekuwa na matukio ya ubakaji hadi kufikia kuitwa “Mji Mkuu wa Ubakaji wa India” ambapo kwa mwaka jana polisi walirekodi zaidi ya matukio 550 ya aina hiyo.
0 comments:
Post a Comment